Tafiti
zimeonesha kuwa kuna uhusiano kati ya ulishaji wa mtoto na
uwezekano
wa kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa utotoni, katika ujana na hata
anapokuwa mtu mzima.Tafiti hizo zimeonyesha kuwa:
•
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama huwakinga watoto dhidi ya kuwa na
uzito
uliozidi na unene uliokithiri wanapokuwa wadogo na hapo baadae.
•
Watoto walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda mfupi (chini ya miezi
sita) na wale waliopewa maziwa mbadala (maziwa ya kopo au ya wanyama)
wako katika hatari zaidi ya kupata baadhi ya magonjwa sugu yasiyoambukizwa
kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na saratani utotoni,
katika ujana na wanapokuwa watu wazima.
•
Ulishaji wa vyakula vya nyongeza vyenye nishati-lishe kwa wingi
unahusishwa
na mtoto kuwa na hatari ya
kupata
unene, saratani na shinikizo kubwa la
damu
ukubwani.

No comments:
Post a Comment
wasiliana nami