Wednesday, 20 August 2014

Jinsi ya kuepuka magonjwa kirahisi

Adhari ya nyama zilizosindikwa
Nyama zilizosindikwa zimethibitishwa
kuongeza hatari ya kupata saratani hata
zikitumiwa kwa kiasi kidogo tu. Nyama
hizi zinahusishwa na saratani za kinywa,
koo, tezi la kiume (prostate), utumbo
mpana na mapafu. Inashauriwa kuepuka kutumia nyama zilizosindikwa. Nyama hizo ni pamoja na zile zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa chumvi, mafuta,kemikali au kukaushwa kwa moshi. Mfano wa nyama hizo ni soseji, nyama za kopo, hot-dog, salami, bacon.

 Umuhimu wa mazoezi ya mwili.
Mazoezi ya mwili ni muhimu kwa binadamu wote, awe mtoto au
mtu mzima, mnene au mwembamba, mgonjwa au mwenye afya njema. Mazoezi
hupunguza uwezekano wa kupata saratani, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo, na shinikizo kubwa la damu. Mazoezi ya mwili pia husaidia kudhibiti
magojwa hayo. Umuhimu mwingine wa mazoezi ya mwili ni kupunguza maumivu ya tumbo yanayotokea wakati wa hedhi, kuzuia ongezeko la uzito wa mwili,kupunguza msongo wa mawazo na pia huboresha afya ya akili ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa kufikiri, kuelewa (cognitive ability) na kukumbuka.


 Kiwango kiitajiwacho kwa mazoezi ya mwili.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu
yasiyoambukizwa, fanya mazoezi ya mwili angalau kwa dakika
30 kila siku. Yaani, dakika 30 za mazoezi yanayotumia
nguvu kiasi kama kutembea kwa haraka (brisk walk).
Unapoanza unaweza kutembea muda mfupi, na baada ya
kuzoea unaweza kuongeza muda hadi dakika 60 kwa siku,
na ukishindwa kabisa kufanya kila siku, fanya angalau
dakika 60 mara tatu kwa wiki.
Namna ya kuongeza mazoezi:
Kama unatumia gari, panga shughuli ambazo
utafanya kila siku kwa kutembea kwa miguu.
Endapo unaishi au kufanya kazi ghorofani jitahidi na
jizoeshe kutumia ngazi kila siku badala ya lifti.
Unapoenda mahali kwa kutembea tumia njia ndefu badala ya njia ya
mkato.
Punguza muda unaotumia kutazama televisheni na utumie muda huo
kufanya shughuli zinazotumia viungo vya mwili kama kufua, kuosha
vyombo, kuosha gari, kusafisha nyumba, kazi za bustani, kufyeka majani.
Ongeza matumizi ya redio, kwani mara nyingi unaweza kufanya shughuli
mbalimbali huku ukisikiliza redio na ikiwezekana uwe na redio ndogo
ambayo unaweza kuihamisha na kuiweka mahali unapofanya shughuli
zako au mazoezi ya mwili.
Watoto wawe na muda wa kucheza kila siku, michezo ambayo inatumia
viungo vya mwili kama kukimbia, kucheza mpira, kuruka kamba nk.
Kumbuka, kila zoezi la mwili unalofanya hata kama ni kidogo sio sawa na
kutofanya kabisa, ni afadhali ufanye kwa kiasi chochote unachoweza kila siku,
halafu uongeze polepole.


No comments:

Post a Comment

wasiliana nami