Monday, 29 September 2014

Athari za uzito ulio kithiri


Uzito uliozidi au unene uliokithiri una uhusiano mkubwa na
magonjwa sugu yasiyoambukizwa. Unene uliokithiri unachangia kwa kiwango
kikubwa kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa kama kisukari, magonjwa ya
moyo, shinikizo kubwa la damu na hata saratani. Unene unachangia katika kuzuia
mwili kutumia sukari kwa ufanisi; pia husababisha kuongezeka kwa mafuta
mwilini ambayo huweza kujikusanya kwenye mishipa ya damu na kufanya damu
isipite kwa urahisi hali ambayo husababisha msukumo mkubwa wa damu. Wakati
mwingine hali hii huweza kusababisha damu isifike kwa kiasi cha kutosha katika
viungo kama moyo, ubongo, misuli n.k. na kuweza kusababisha magonjwa ya
moyo kama moyo kushindwa kufanya kazi kabisa (heart failure) au moyo kukosa
damu ya kutosha (ischemic heart disease).

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami