Wednesday, 11 February 2015

Fahamu ugojwa wa kisukari



Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu.Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati-lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na chakula huhitaji kichocheo cha insulini. Kichocheo hiki
hutengenezwa na kongosho.Kichocheo cha insulini ndicho kinachodhibiti kiwango cha sukari katika damu.Wakati kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo cha insulini au insulini iliyopo katika damu inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi husababisha ugonjwa wa kisukari.

Kuna aina mbili kuu za kisukari ambazo ni 
kisukari kinachotegemea insulini
(type 1 diabetes) na 
kile kisichotegemea insulini (type 2 diabetes):
• Kisukari kinachotegemea insulini (type1 diabetes)huwapata zaidi watoto.
Katika aina hii ya kisukari, seli za kongosho zinazotengeneza insulini
huwa zimeharibika na hivyo kusababisha upungufu au ukosefu wa
insulini.
• Kisukari kisichotegemea insulini (type 2 diabetes) huwapata zaidi watu
wenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea. Katika aina hii ya kisukari,insulini ya kutosha inaweza ikatengenezwa katika kongosho lakini haifanyi kazi na hivyo mwili hushindwa kutumia sukari kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami