Monday, 18 August 2014

Waliokimbia zahanati ya ebola watafutwa


Ebola  Liberia
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku..
Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine.
Mwandishi  katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami