Chumvi inapotumika kwa kiasi kidogo haina madhara. Miili yetu
chini
ya gramu 5 (kijiko cha chai) kwa siku. Hii Huupatia mwili madini ya
sodium
yanayohitajika kwa siku. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba mwili
unapata
pia madini haya kutoka kwenye vyakula vingine, hivyo chumvi itumike kwa
kiasi kidogo. Kwa bahati mbaya tunatumia chumvi kupita kiasi. Matumizi ya
chumvi nyingi yanaongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu,kwani
chumvi husababisha maji kujikusanya mwilini. Maji yaliyojikusanya huongeza
shinikizo kwenye moyo na mishipa ya damu na hivyo kusababisha moyo kufanya
kazi
kwa nguvu zaidi. Shinikizo kubwa la damu huongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo, na pia ya mifupa
kwa nguvu zaidi. Shinikizo kubwa la damu huongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengine sugu kama yale ya figo, moyo, na pia ya mifupa
kama
“osteoporosis”. Hivi karibuni tafiti zimeonyesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi
ya vyakula vilivyosindikwa au kuhifadhiwa kwa chumvi na saratani ya tumbo.
Hivyo ni muhimu kupunguza matumizi ya chumvi.
Jinsi ya kupunguza matumizi ya chumvi
kupunguza
uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa sugu.
Yafuatayo
yatasaidia kufikia lengo hilo:
•
Punguza chumvi inayowekwa kwenye chakula wakati wa
kupika.
•
Usiongeze chumvi katika chakula wakati wa kula, pia
usiweke chumvi
mezani.
Mara nyingi watu huongeza chumvi bila hata kuonja chakula.
•
Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa kutumia au kuongezwa
chumvi,
kama
nguru aliyekaushwa kwa chumvi, baadhi ya vyakula vya makopo
au
paketi, (kama supu za paketi au makopo, “soy souce” michanganyiko
ya
kunogesha mchuzi, crisps). Ni vyema kusoma lebo kwa makini na
chagua
vyakula vilivyoandikwa “hakuna chumvi iliyoongezwa”(“no salt
added”)
•
Tumia zaidi vyakula freshi unavyopika mwenyewe kwani
unaweza
kuthibiti
kiasi cha chumvi unachotumia.
•
Tumia zaidi viungo kuongeza ladha kwenye chakula,
mfano vitunguu
saumu,
tangawizi n.k.
Kama
umezoea kutumia chumvi nyingi inaweza kuchukua muda kidogo
kujizoesha
kula chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi. Jizoeshe
taratibu
mpaka uzoee na mwisho utafurahia vyakula vyenye chumvi kidogo au
visivyo
na chumvi.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami