Bofya hapa
Vipimo vya ebola vyafanyika baada ya kifo cha abilia huko nchini uingereza
Abilia huyo aliyekuwa akitokea nchini Gambia alifariki dunia alipowasili katika uwanja wa ndege huko nchini Uingereza .
Taarifa zinaonyesha kuwa watu 728 wamefariki dunia kwa Ebola huko Guinea, Liberia na Sierra Leone mwaka huu,baada ya kuzuka kwa ugonjwa huu. Licha ya kuwepo kwa tukio kama hilo bado Uingereza haijaingia katika hali ya hatari Zaidi kuhusu ugonjwa huu.'
Dalili za ugonjwa huu
Virusi vya Ebola huenea kwa njia ya mawasiliano ya binadamu na kupitia majimaji yaliyo ndani ya mwili wa mgonjwa.
Dalili kama za homa ya awali inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi kupitia maeneo kama macho na ufizi.
- homa ya juu, kutokwa na damu na uharibifu mfumo mkuu wa neva
- Kiwango cha vifo inaweza kufikia 90%
- Kipindi cha dalili za mwanzo ni siku 2 hadi 21
- Hakuna chanjo au tiba
muuguzi akipuliza dawa katika kitengo cha kutengwa huko Liberia
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami