Ni
muhimu kula mbogamboga na matunda kwa wingi kila siku, na hasa wakati
wa mlo. Unashauriwa kula mbogamboga na matunda ya rangi mbalimbali kwani
rangi zinapokuwa za aina mbalimbali ubora huongezeka.Inashauriwa
kutumia angalau vipimo vitano vya mbogamboga na matunda
kila siku. Mfano wa kipimo kimoja ni kama ifuatavyo:
kikombe
kimoja cha chai (250mls);
•
Mboga za majani zilizopikwa kama mchicha au matembelekiasi
•
Mboga zisizopikwa (kachumbari/ saladi) - bakuli moja
kubwa
ujazo unaoweza kuchukua mlo wa mtu mmoja;
•
Chungwa moja;
•
Ndizi mbivu kubwa kiasi - moja;
•
Tikiti- maji kipande kikubwa kimoja
•
Parachichi moja dogo;
•
Mapera mawili;
•
Juisi glasi moja (250mls)
Mfano: Kwa siku moja (asubuhi
hadi usiku) unaweza kula kama ifuatavyo, na
isambazwe
katika siku nzima: glasi moja juisi, mapera mawili, mchicha uliopikwa
kiasi
cha ujazo wa kikombe kimoja cha chai (250mls), matembele yaliyopikwa
kiasi
cha ujazo wa kikombe kimoja cha chai (250mls) saladi bakuli moja.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami