Uzito
uliozidi au unene uliokithiri una uhusiano mkubwa na
magonjwa
sugu yasiyoambukizwa. Unene uliokithiri unachangia kwa kiwango
kikubwa
kupata magonjwa sugu yasiyoambukizwa kama kisukari, magonjwa ya
moyo,
shinikizo kubwa la damu na hata saratani. Unene unachangia katika kuzuia
mwili
kutumia sukari kwa ufanisi; pia husababisha kuongezeka kwa mafuta
mwilini
ambayo huweza kujikusanya kwenye mishipa ya damu na kufanya damu
isipite
kwa urahisi hali ambayo husababisha msukumo mkubwa wa damu. Wakati
mwingine
hali hii huweza kusababisha damu isifike kwa kiasi cha kutosha katika
viungo
kama moyo, ubongo, misuli n.k. na kuweza kusababisha magonjwa ya
moyo
kama moyo kushindwa kufanya kazi kabisa (heart failure) au moyo kukosa
damu
ya kutosha (ischemic heart disease).