Monday, 29 September 2014

sababu za kupata uzito ulio kithiri.


Uzito wa mwili hutegemea kiasi na aina ya chakula unachokula
pamoja na shughuli unazofanya. Mara nyingi unene hutokana na kula chakula
kwa wingi kuliko mahitaji ya mwili na kutofanya mazoezi. Mahitaji ya chakula
mwilini hutegemea umri, jinsi; hali ya kifiziologia uliyonayo (kama una ujauzito
au unanyonyesha), kazi na mtindo wako wa maisha. Endapo kiasi cha chakula
unachokula kinatoa nishati – lishe kuliko mahitaji ya mwili, ziada hii huhifadhiwa

mwilini kama mafuta hivyo kuongezeka kwa uzito wa mwili.

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami