Wednesday, 19 November 2014

Shinikizo kubwa la damu ni nini?


Shinikizo kubwa la damu hutokea panapokuwa na ongezeko la
nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye
moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini. Ukubwa wa shinikizo
hilo la damu unategemea wingi na nguvu ya msukumo wa damu
kutoka kwenye moyo na ukubwa wa mishipa inayopeleka damu
mwilini. Katika vituo vya tiba kifaa maalum hutumika kupima
shinikizo la damu na kiwango kinachochukuliwa kuwa
cha kawaida ni 120/80 mmHg au chini yake. Pale kiwango
kinapokuawa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni
shinikizo kubwa la damu, kama inavyoelezwa katika mwongozo
wa viwango vya shinikizo la damu. Hata hivyo panaweza kuwepo
tofauti kati ya mtu na mtu.
DALILI ZA SHINIKIZO KUBWA LA DAMU.
Kwa kawaida hakuna dalili za wazi zinazojitokeza pale ambapo una
shinikizo kubwa la damu. Utafahamu kama una shinikizo kubwa la damu kwa
kufanyiwa kipimo katika kituo cha tiba. Endapo shinikizo lako la damu litakuwa
liko kiwango cha juu sana unaweza ukaumwa kichwa mara kwa mara hasa
sehemu ya kisogo, ukapata kizunguzungu, ukatokwa na damu puani, ukapata
maumivu ya kifua, moyo kwenda kasi wakati umepumzika, ukashindwa kufanya
mazoezi kwani utashindwa kupumua, kuyasikia mapigo ya moyo wako wakati
umepumzika na kupata uchovu wa mara kwa mara.
Jedwali la mwongozo wa viwango vya shinikizo la damu
Shinikizo la damu Kiwango cha shinikizo la damu
Kiwango cha kawaida 120/80 au chini yake
Kiashiria cha mwanzo wa shinikizo
kubwa la damu
Kati ya 121/80 na 139/89
Shinikizo kubwa la damu 140/90 au Zaidi
Kwa bahati mbaya watu wengi huishi na tatizo hili kwa muda mrefu bila
kufahamu kwani hakuna dalili zilizo bayana. Mara nyingi shinikizo kubwa la
damu hutambulika pale unapokwenda kituo cha huduma ya afya kupima afya
yako au kupata matibabu ya tatizo jingine la kiafya. Hali hii humweka mtu
katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya
kupima afya yako mara kwa mara.


Tuesday, 4 November 2014

Kwanini uhumie na msongo wa mawazo,,!!!!!!

Msongo wa mawazo ni aina ya hisia inayojitokeza ili kukabiliana
na matukio, changamoto au hali mbalimbali za kimaisha. Hisia hiyo huweza kuamshwa na matukio mbalimbali kama vile kufiwa na mtu wa
karibu, kukabiliwa na tatizo katika familia, maisha au shuleni; kuwa na kazi
nyingi kwa muda mrefu bila ya kuwa na muda wa kupumzika n.k. Hisia hizo
zinaweza kusababisha hasira, wasiwasi, woga, huzuni, kuchanganyikiwa au pia kukata tamaa. Msongo wa mawazo ukijitokeza mara kwa mara kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya kiafya.
Athari za msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huweza

Monday, 3 November 2014

Zifahamu athari za uvutaji wa sigara



 Kaa mbali na mvuta sigara

mtu asiyevuta sigara aliyekaa karibu na mvutaji. Tafiti mbalimbali zinaonesha
kuwa moshi wa sigara kwa mtu asiyevuta huweza kusababisha magonjwa ya
moyo, magonjwa ya njia ya hewa, maumivu ya macho na pua, kuumwa kichwa
na kichefuchefu. Kwa mwanamke mjamzito asiyevuta, moshi wa sigara huweza
kusababisha kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu.

Kwa watoto moshi wa sigara huweza kusababisha magonjwa ya njia ya hewa
(kama asthma, nimonia na kikohozi cha kudumu), magonjwa katika njia ya sikio
na maendeleo hafifu ya ukuwaji wao kimwili na kiakili.

Athari za sigara kwa mama mjamzito

Mwanamke mjamzito akivuta sigara au akitumia tumbaku mtoto
aliye tumboni huathirika na sumu iliyopo ndani ya sigara au tumbaku, hivyo
kuweza kusababisha yafuatayo:
Mtoto kuzaliwa na uzito pungufu na umbile dogo;
Mtoto kuzaliwa kabla ya siku zake yaani njiti;
Mtoto kudumaa;
Mtoto kuwa taahira; na
Mtoto huweza kufariki ghafla katika mwaka wa kwanza wa maisha
yake.