Tuesday, 4 November 2014

Kwanini uhumie na msongo wa mawazo,,!!!!!!

Msongo wa mawazo ni aina ya hisia inayojitokeza ili kukabiliana
na matukio, changamoto au hali mbalimbali za kimaisha. Hisia hiyo huweza kuamshwa na matukio mbalimbali kama vile kufiwa na mtu wa
karibu, kukabiliwa na tatizo katika familia, maisha au shuleni; kuwa na kazi
nyingi kwa muda mrefu bila ya kuwa na muda wa kupumzika n.k. Hisia hizo
zinaweza kusababisha hasira, wasiwasi, woga, huzuni, kuchanganyikiwa au pia kukata tamaa. Msongo wa mawazo ukijitokeza mara kwa mara kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya kiafya.
Athari za msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huweza
kusababisha ulaji na unywaji usiofaa, pia huweza
kuleta mfadhaiko, kuumwa na kichwa au shinikizo
kubwa la damu. Msongo wa mawazo pia humuweka
mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na
kiharusi.
Dalili za msongo wa mawazo ni pamoja na kukosa
usingizi, kukosa hamu ya kula au kula sana, kunywa
pombe kuzidi kipimo, kukosa hamu ya kufanya
shughuli yoyote hata mazoezi na pia kuvuta sigara,
kutumia mihadarati au madawa ya kulevya.
Inashauriwa kuwa ili kupunguza msongo wa mawazo unapaswa kuwa na tabia
ya kufanya mazoezi, kujipa muda wa kupumzika, kushiriki katika shughuli
mbalimbali za kijamii kama michezo, tamasha, harusi na matukio mengine
yanayofurahisha na yaliyo salama. Ni muhimu pia kupangilia vizuri matumizi
ya muda wako. Mara nyingine husaidia endapo utamweleza mtu unayemwamini
matatizo yanayokusibu ili kuweza kupata ushauri au faraja. Ni bora kusema

HAPANA mambo yanapozidi uwezo na pata muda wa kupumzika.

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami