Ni kweli kwamba moshi wa sigara au tumbaku huweza kumuathiri kiafya mtu
asiyevuta sigara aliyekaa karibu na mvutaji. Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa
moshi wa sigara kwa mtu asiyevuta huweza kusababisha magonjwa ya moyo,
magonjwa ya njia ya hewa, maumivu ya macho na pua, kuumwa kichwa
na
kichefuchefu. Kwa mwanamke mjamzito asiyevuta, moshi wa sigara huweza kusababisha
kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu. Kwa
watoto moshi wa sigara huweza kusababisha magonjwa ya njia ya hewa
(kama
asthma, nimonia na kikohozi cha kudumu), magonjwa katika njia ya sikio na
maendeleo hafifu ya ukuwaji wao kimwili na kiakili.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami