Saturday, 30 August 2014

Ebola yaenea katika kitovu cha mafuta Nigeria


Kifo cha daktari huyo ni cha kwanza kutokea nje ya mji wa Lagos
Serikali ya Nigeria imethibitisha kutokea kifo cha daktari mmoja kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mji wa Port Harcout nje ya mji wa Lagos.
Watu wengine zaidi ya sabini wanachunguzwa mjini humo huku mke wa daktari huyo akiwekwa katika chumba chake kando kufanyiwa uchuguzi zaidi.
Daktari huyo alimtibu mgonjwa wa Ebola ambaye alifanikiwa kupona.
Mwanamume huyo inaarifiwa alikutana na Patrick Sawyer, mwanamume aliyeeneza Ebola kutoka Liberia hadi Nigeria.
Mawaziri wa afya katika kanda ya Afrika Magharibi wanakutana baadaye leo kujadili njia za kupambana na Ebola, ugonjwa ambao umetikisa dunia nzima, hususan kanda ya Afrika Magharibi.
Zaidi ya watu1,550 wamefariki, wengi chini, Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Waziri wa afya wa Nigeria Onyebuchi Chukwu, amesema kuwa daktari aliyefariki mjini Port Harcourt, alifariki tarehe 22 lakini matokeo ya uchunguzi wa kilichomuua yametangazwa hivi karibuni.
Daktari huyo ni mtu wa sita kufariki kutokana na Ebola nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu Afrika.

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami