Kuna hofu kwamba mlipuko wa
ugonjwa wa Ebola, katika kanda ya Afrika Magharibi, utaendelea kuwa
mbaya zaidi hadi kanda hiyo itakapopata afueni kutokana na ugonjwa huo.
Hii ni kwa mujibu wa maafisa wakuu wa afya nchini Marekani.Mawaziri wa afya katika kanda hiyo wanatarajiwa kukutana nchini Ghana kujadili hali ya ugonjwa huo ambayo inaendelea kuleta wasiwasi.
Shirika la afya duniani linasema kuwa ugonjwa huo umewaua watu 1,427.
Shirika hilo linasema kuwa huu ndio mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo kuwahi kushudiwa na umewaathiri watu 2,615.
Bwana Frieden, alikutana na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kujadili njia za kupmbana na ugonjwa huo.
''Visa vya maambukizi vinaongezeka.Ni jambo la kusikitisha, lakini hivi ndivyo hali ilivyo, na huenda ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo,'' alisema Bwana Frieden.
Mlipuko wa Ebola kama huu haujawahi kushuhudiwa. Kadhalika licha ya idadi ya walioambukizwa kuwa kubwa, tunafahamu kuwa kuna watu wengi zaidi walioambaukizwa na visa hivyo vimeripotiwa, '' aliongeza kusema bwana Frieden.
Alielea kwamba kuna umuhimu wa hatua za dharura kuchukuliwa na kuwataka wananchi wa Liberia kushirikiana kupambana na ugonjwa huo na pia kuachana na mienendo ambayo imechochea kuenea ugonjwa huo.
Licha ya fununu kwamba virusi vya homa hiyo havienezwi kupitia hewani na maji maji ya mwilini, kama vile damu au jasho, kutoka kwa wale walioambukizwa.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami