Shirika la afya duniani WHO
limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi huenda
ukasambaa na kuwaambukiza zaidi ya watu 20,000 kabla haujadhibitiwa.
Kwa sasa idadi ya waliothibitishwa na
kuorodheshwa kuambukizwa ni elfu 3 ingawaje inashukiwa kuna wengi
wengine ambao hawajajulikana.Mkurugenzi wa WHO katika kanda hiyo - Dr Lious Sambo - ameeelezea jinsi wafanyikazi katika kliniki za wagonjwa wanavyo'ng'ang'ana wakijaribu kukabilianana na janga hilo la Ebola.
Wauguzi ni wachache ilihali wanapaswa kusaidia haraka inavyowezekana
Wagonjwa watano wa Ebola pia wamefariki Nigeria .
Mawaziri wa afya katika eneo hilo la Afrika magharibi wanakutana nchini GHana kujadili janga hilo.
Mkurugenzi wa MSF huko Liberia, Brice de la Vigne, ameiambia BBC vitanda zaidi ya elfu vinahitajika huko Liberia kwa minajili ya kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami