Sunday, 12 October 2014

Pombe mbaya jamani, ebu muoni huyu.



Kama hunywi pombe unayo sababu ya kufurahi sana, na kamwe usianze kunywa pombe. Kama
unakunywa pombe, punguza sana na ukiweza acha kabisa.
Hii ni kwa sababu tafiti zinaendelea kuthibitisha kwamba pombe ina madhara mengi kiafya, ikiwa ni pamoja na kusababisha magonjwa, kupunguza uwezekano wa ini kufanya kazi vizuri na pia huathiri uwekaji wa akiba za virutubishi mwilini.
Imethibitishwa kwamba pombe inaongeza sana uwezekano wa kupata saratani hasa ya kinywa, koo, koromeo, matiti, utumbo mkubwa na ini.
Pombe husababisha ongezeko la uzito wa mwili. Unene pia huongeza uwezekano wa kupata aina nyingi za saratani na magonjwa mengine sugu yasiyoambukizwa,ikiwemo kisukari, ugonjwa wa moyo, shinikizo kubwa la damu na kiharusi.

 Athari za sigara
Uvutaji wa sigara, utumiaji wa tumbaku na bidhaazake huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo, saratani,

(hasa za mapafu, kinywa na koo), magonjwa sugu mengine ya njia ya hewa, shinikizo kubwa la damu na vidonda vya tumbo.
Sumu iliyopo katika sigara (nicotine), huharibu ngozi ya ndani
ya mishipa ya damu hivyo huongeza uwezekano wa lehemu kujikusanya kwenye sehemu za mishipa ya damu zilizoathiriwa.
inavyotakiwa. Sigara pia huongeza kiasi cha chembechembe haribifu
Nicotine huweza pia kusababisha mishipa ya damu kuziba au kuwa myembamba kuliko kawaida na hivyo kuzuia damu kupita
(free radicals) mwilini. Matumizi ya sigara pia huweza kuleta athari kwa wale
walio karibu na mvutaji.
Ili kuzuia matatizo haya ni muhimu kuepuka kuvuta sigara na matumizi ya
tumbaku na bidhaa zake.
 

Friday, 10 October 2014

Jinsi ya kutambua usahihi wa uzito wako.



Uzito wa mtu hutegemea umri na jinsia; hivyo viashiria mbalimbali hutumika ili kuweza kutambua uzito unaotakiwa kuwa nao au hali yako ya lishe. Njia rahisi inayotumika kwa watu wazima (isipokuwa wanawake
wajawazito) ni ile ya kuangalia uwiano wa uzito na urefu wa mtu yaani “body mass index (BMI)” au fahirisi ya uzito wa mwili (FUM) ambayo hutumia viwango mbalimbali kutathmini hali ya lishe ya muhusika. Kanuni ifuatayo hutumika kupata BMI:
BMI = Uzito (kilo)
Urefu (mita) ²
BMI huwa na viwango mbalimbali vinavyoashiria hali ya lishe ya mtu.
Ifuatayo ni tafsiri ya viwango hivyo kama ilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani:
BMI chini ya 18.5 = Hali duni ya lishe
BMI kati ya 18.5 mpaka 24.9 = Hali nzuri ya lishe
BMI kati ya 25.0 na 29.9 = Unene uliozidi
BMI ya 30.0 au zaidi = Unene uliokithiri au kiribatumbo.


Kipimo kingine kinachoweza kuonyesha kama una uzito uliozidi au unene ni kipimo cha mzunguko wa kiuno. Kipimo hiki husaidia kuonyesha kiasi cha mafuta kilichohifadhiwa tumboni. Kuwa na mafuta mengi sehemu ambazo ni karibu na moyo ni hatari zaidi ukilinganisha na mafuta yaliohifadhiwa sehemu nyingine za mwili. Umbile la mwili huweza kuashiria hatari hiyo. Umbile la mwili linalojulikana kama “pear shape” mafuta huhifadhiwa hasa kwenye makalio, ambapo “apple shape” mafuta huhifadhiwa zaidi tumboni. Hivyo mtu
mwenye “apple shape” huwa katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kiafya.Mzunguko wa kiuno hupimwa kwa kuzungusha utepe wa kupimia (futi-kamba) kupitia mfupa wa nyonga kwa kufuata hatua zifuatazo:
1. Ili kuhakikisha usahihi wa vipimo usijipime mwenyewe.