Kama
hunywi pombe unayo sababu ya kufurahi sana,
na kamwe usianze kunywa pombe. Kama
unakunywa
pombe, punguza sana na ukiweza acha kabisa.
Hii
ni kwa sababu tafiti zinaendelea kuthibitisha kwamba pombe
ina madhara mengi kiafya, ikiwa ni pamoja na kusababisha
magonjwa, kupunguza uwezekano wa ini kufanya kazi
vizuri na pia huathiri uwekaji wa akiba za virutubishi mwilini.
Imethibitishwa
kwamba pombe inaongeza sana uwezekano wa kupata
saratani hasa ya kinywa, koo, koromeo, matiti, utumbo mkubwa na ini.
Pombe
husababisha ongezeko la uzito wa mwili. Unene pia huongeza uwezekano wa
kupata aina nyingi za saratani na magonjwa mengine sugu yasiyoambukizwa,ikiwemo
kisukari, ugonjwa wa moyo, shinikizo kubwa la damu na kiharusi.
Athari za sigara
Uvutaji
wa sigara, utumiaji wa tumbaku na bidhaazake
huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo, saratani,
(hasa
za mapafu, kinywa na koo), magonjwa sugu mengine ya njia
ya hewa, shinikizo kubwa la damu na vidonda vya tumbo.
Sumu
iliyopo katika sigara (nicotine), huharibu ngozi ya ndani
inavyotakiwa.
Sigara pia huongeza kiasi cha chembechembe haribifu
Nicotine huweza pia kusababisha
mishipa ya damu kuziba au kuwa
myembamba kuliko kawaida na hivyo kuzuia damu kupita
(free
radicals) mwilini. Matumizi ya sigara pia huweza kuleta athari kwa wale
walio
karibu na mvutaji.
Ili
kuzuia matatizo haya ni muhimu kuepuka kuvuta sigara na matumizi ya
tumbaku
na bidhaa zake.
No comments:
Post a Comment
wasiliana nami