Friday, 10 October 2014

Jinsi ya kutambua usahihi wa uzito wako.



Uzito wa mtu hutegemea umri na jinsia; hivyo viashiria mbalimbali hutumika ili kuweza kutambua uzito unaotakiwa kuwa nao au hali yako ya lishe. Njia rahisi inayotumika kwa watu wazima (isipokuwa wanawake
wajawazito) ni ile ya kuangalia uwiano wa uzito na urefu wa mtu yaani “body mass index (BMI)” au fahirisi ya uzito wa mwili (FUM) ambayo hutumia viwango mbalimbali kutathmini hali ya lishe ya muhusika. Kanuni ifuatayo hutumika kupata BMI:
BMI = Uzito (kilo)
Urefu (mita) ²
BMI huwa na viwango mbalimbali vinavyoashiria hali ya lishe ya mtu.
Ifuatayo ni tafsiri ya viwango hivyo kama ilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani:
BMI chini ya 18.5 = Hali duni ya lishe
BMI kati ya 18.5 mpaka 24.9 = Hali nzuri ya lishe
BMI kati ya 25.0 na 29.9 = Unene uliozidi
BMI ya 30.0 au zaidi = Unene uliokithiri au kiribatumbo.


Kipimo kingine kinachoweza kuonyesha kama una uzito uliozidi au unene ni kipimo cha mzunguko wa kiuno. Kipimo hiki husaidia kuonyesha kiasi cha mafuta kilichohifadhiwa tumboni. Kuwa na mafuta mengi sehemu ambazo ni karibu na moyo ni hatari zaidi ukilinganisha na mafuta yaliohifadhiwa sehemu nyingine za mwili. Umbile la mwili huweza kuashiria hatari hiyo. Umbile la mwili linalojulikana kama “pear shape” mafuta huhifadhiwa hasa kwenye makalio, ambapo “apple shape” mafuta huhifadhiwa zaidi tumboni. Hivyo mtu
mwenye “apple shape” huwa katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kiafya.Mzunguko wa kiuno hupimwa kwa kuzungusha utepe wa kupimia (futi-kamba) kupitia mfupa wa nyonga kwa kufuata hatua zifuatazo:
1. Ili kuhakikisha usahihi wa vipimo usijipime mwenyewe.
2. Hakikisha mtu anayepimwa amevua nguo zote isipokuwa nguo nyepesi za
ndani. Nguo zote zinazobana zivuliwe.
3. Hakikisha mtu anayepimwa amesimama akiwa amenyooka na miguu yake
iwe pamoja na asiegemee upande mmoja. Apumue kama kawaida na vipimo
vyake vichukuliwe akiwa anatoa pumzi. Hali hii huwezesha misuli ya tumbo
kulegea na hivyo kuweza kupata vipimo sahihi.
4. Mpimaji asimame pembeni mwa mtu anayepimwa na azungushe utepe
wa kupimia kuanzia kwenye mfupa wa nyonga na kukutanisha utepe huo
tumboni, usawa wa kitovu. Hakikisha utepe haubani lakini pia haulegei.
5. Vipimo vichukuliwe na kurekodiwa katika kadirio la karibu la nusu sentimita
(0.5).
Tafsiri ya vipimo:
Mwanamke: Mzunguko usizidi sentimita 88
Mwanamme: Mzunguko usizidi sentimita 102
Chukua hatua ya kutafuta ushauri wa mtaalam wa afya au lishe iwapo
mzunguko wa kiuno ni mkubwa kuliko viwango vilivyopendekezwa na
Shirika la Afya Duniani (WHO).

No comments:

Post a Comment

wasiliana nami