Saturday, 30 August 2014

Mawaziri wa Afya wajadili Ebola


Mtu akisoma tangazo kuhusu onyo dhidi ya maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa Ebola mjini Monrovia, Liberia.
Mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Magharibi wamekubaliana kuondoa upigaji marufuku wa safari za ndege na ufungaji wa mipaka kwa nchi ziliathirika kutokana na ugonjwa wa Ebola. Mawaziri hao ambao wamekutana mjini Accra, Ghana kupitia upya mikakati iliyokuwa ikitumika kupambana na virusi vya ebola

WHO:Hofu ya 20,000 kuambukizwa Ebola


Mawaziri wa afya wa Afrika Magharibi wanakutana Ghana kutafita njia za kupambana na Ebola
Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi huenda ukasambaa na kuwaambukiza zaidi ya watu 20,000 kabla haujadhibitiwa.

Njia 5 za kuepuka virusi hatari vya Ebola


Njia za kuepuka kuambukizwa Ebola
Ebola:Njia tano za kujiepusha virusi hatari vya homa ya Ebola
Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
1. Sabuni na maji
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye

Ebola:Hofu yaendelea kutanda A.Magharibi


Liberia ni baadhi ya nchi zilizoathirika sana kutokana na Ebola
Kuna hofu kwamba mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, katika kanda ya Afrika Magharibi, utaendelea kuwa mbaya zaidi hadi kanda hiyo itakapopata afueni kutokana na ugonjwa huo.
Hii ni kwa mujibu wa maafisa wakuu wa afya nchini Marekani.
Mkurugenzi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa , Tom Frieden,amesema kuwa ugonjwa huo unahitaji hatua zaidi ili kuweza kuudhibiti.

Ebola yaenea katika kitovu cha mafuta Nigeria


Kifo cha daktari huyo ni cha kwanza kutokea nje ya mji wa Lagos
Serikali ya Nigeria imethibitisha kutokea kifo cha daktari mmoja kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mji wa Port Harcout nje ya mji wa Lagos.
Watu wengine zaidi ya sabini wanachunguzwa mjini humo huku mke wa daktari huyo akiwekwa katika chumba chake kando kufanyiwa uchuguzi zaidi.
Daktari huyo alimtibu mgonjwa wa Ebola ambaye alifanikiwa kupona.

Mafuta yaliyo bora kwa afya


Mafuta ni muhimu mwilini, isipokuwa yanahitajika kwa kiasi
kidogo; hivyo kuepuka kabisa ulaji wa mafuta huweza kuleta
athari katika mwili, ikiwemo ubongo kutofanya kazi vizuri. Hata hivyo mafuta
yanapotumiwa kwa kiasi kikubwa yanaweza kuleta madhara mwilini. Hivyo ni
muhimu kuwa makini na kiasi cha mafuta kinacholiwa katika kila mlo.

Friday, 22 August 2014

Africa kusini yafunga Mipaka yake

Nchi ya Africa Kusini inafunga mipaka yake kwa wasafiri kutoka katika nchi za Liberia,Guine na Sierra Leone nchi hizo tatu zimeathiriwa vibaya na mripuko wa ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa Afya wa taifa hilo, Aaron Motsoaledi,amesema kwamba marufuku hiyo haiwahusu raia wa nchi hiyo ingawa watalazimika kukaguliwa kitabibu ili kubaini endapo watakuwa wamepata

Thursday, 21 August 2014

Vitongoji hivyo vilivyoathirika na ugonjwa wa Ebola vya andamana huko Liberia


Maafisa wa usalama wakiwa Westpoint baada ya uvamizi wa kituo cha Ebola
Polisi nchini Liberia wamerusha vitoa machozi kuwatawanya umati uliojaa hasiria katika mji mkuu Monrovia wakipinga kuzingirwa kwa kitongoji chao na maafisa wa Usalama.
Maafisa wa usalama walilazimika kutumia nguvu baada ya waandamanaji kuanza kuwapura kwa mawe katika kitongoji cha Westpoint .

Wednesday, 20 August 2014

Serikali yatakiwa kupeleka vifaa vya kutambua ebola Tunduma

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Seleman Rashid.
Serikali imeombwa kupeleka haraka vifaa vyenye uwezo wa kuwatambua watu wenye maambukizi ya ugonjwa wa ebola katika mpaka wa Tanzania na Zambia mjini Tunduma ili kuepusha ugonjwa huo kuingia nchini kirahisi kwa kupitia katika mpaka huo.

Mpaka huo unatumiwa na nchi zaidi ya sita za Kusini mwa Afrika.

Ombi hilo lilitolewa na baadhi ya wakazi wa mji wa Tunduma kuhusiana na tahadhari inayoweza kuchukuliwa ili kuepusha ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuenea katika nchi za Afrika Magharibi kuingia nchini.

Wananchi hao pia wameitaka serikali kuanza kutoa elimu kwa wananchi wanaoshi maeneo ya mipakani juu ya dalili za ugonjwa huo ili iwe rahisi kwao kujikinga na kutoa taarifa punde wanapomuona mtu mwenye dalili za kuugua ugonjwa huo.

Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka, alisema kuwa hadi sasa, hakuna elimu iliyotolewa kwa wananchi juu ya ugonjwa huo wala tahadhari iliyochukuliwa na serikali kwa wageni wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Tunduma.

“Mpaka sasa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na serikali kuwakinga Watanzania wasipatwe na maambukizi ya ebola kutoka kwa wageni wanaoingia nchini kupitia mpaka huu," alisema.

Naye Samwel Mkisi, mkazi wa Tunduma, alisema ugonjwa huo wanausikia tu kupitia kwenye vyombo vya habari.

Kaimu Ofisa Afya katika mpaka wa Tunduma, Jamal Mohamed, alisema kazi ya kuwapima wageni wanaoingia na kutoka ili kutambua kama wana maambukizi ya ebola, bado haijaanza kutokana na kutokuwapo kwa vifaa.

Hata hivyo, alisema kuwa tayari serikali imevituma vifaa hivyo kutoka Dar es Salaam na kwamba kazi ya upimaji itaanza mara moja.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mipakani mkoani Mbeya ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, Lusarago Mleka, alisema kutokana na kutokuwapo kwa udhibiti wa kiafya, kunasababisha watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kwa hofu.

Jinsi ya kuepuka magonjwa kirahisi

Adhari ya nyama zilizosindikwa
Nyama zilizosindikwa zimethibitishwa
kuongeza hatari ya kupata saratani hata
zikitumiwa kwa kiasi kidogo tu. Nyama
hizi zinahusishwa na saratani za kinywa,
koo, tezi la kiume (prostate), utumbo
mpana na mapafu. Inashauriwa kuepuka kutumia nyama zilizosindikwa. Nyama hizo ni pamoja na zile zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa chumvi, mafuta,kemikali au kukaushwa kwa moshi. Mfano wa nyama hizo ni soseji, nyama za kopo, hot-dog, salami, bacon.

Ebola:Wagonjwa 17 waliokuwa wametoroka katika kituo cha Monrovia wapatikana


Mmoja wa wanaume waliovamia kituo hicho na kumbeba mgonjwa
Waziri wa habari wa Liberia Lewis Brown amesema kuwa wagonjwa wote 17 wa Ebola waliokuwa wametoweka kutoka kwa kituo cha kuwatenga na umma wamepatikana.
Kupatikana kwao imekamilisha idadi ya wote 37 waliokuwa katika zahanati iliyovamiwa na wenyeji jumamosi iliyopita.
Wagonjwa 37 walikuwa katika kituo hicho cha Ebola kilichoko karibu na kitongoji cha WestPoint Viungani mwa

Monday, 18 August 2014

Albino akatwa kiungo Tabora

Matukio ya kukata viungo vya walemavu wa ngozi (albino), yameendelea mkoani hapa, ambapo juzi mlemavu wa pili katika muda usiozidi wiki mbili, amekatwa kiwiko cha mkono wake na wahusika kutoweka nacho kusikojulikana. soma zaidi

Waliokimbia zahanati ya ebola watafutwa


Ebola  Liberia
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku..

Sunday, 17 August 2014

Rais wa Colombia aunga mkono Bhangi



Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Rais wa Colombian Juan Manuel Santos amesema kuwa anaunga mkono matumizi ya bangi kwa minajili ya utabibu.
Bwana Santos ameunga mkono mswada ambao utapigiwa kura bungeni wakati wowote kwa manufaa ya kupunguza uchungu kwa wagonjwa .
Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Rais huyo amesema kuwa kuhalalishwa kwa Bangi kutawanyima walanguzi wa mihadarati biashara kwani itakuwa sio haramu kupatikana na bangi nchini humo.
Colombia ni moja kati ya mataifa ambayo yamekumbwa na vita vya walanguzi wa madawa ya kulevya na serikali vita ambavyo vimesababisha mauaji ya mamia ya watu. .
Marijuana inakuzwa kwa wingi nchini Colombia, lakini taifa hilo linajulikana kote duniani kwa ukuaji wa cocaine, kwa pamoja na Peru.
Bhangi inakuzwa kwa wingi nchini Colombia
Asilimia kubwa ya madawa hayo kulingana na takwimu yanauzwa nchini Marekani ambapo yanaingizwa kisirisiri kupitia mataifa ya Marekani ya kati na Mexico.
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema bwa Santos akiwa mjini Bogota

Ebola haijaingia nchini - Waziri

Wagonjwa waliohisiwa wamepimwa hawajaambukizwa
.
Wakati hofu ya kuingia kwa ugonjwa wa Ebola nchini ikiwa imetanda, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema hadi sasa hakuna wagonjwa waliobainika kuwa nao.

Juzi wagonjwa wawili, mmoja akiwa raia wa Benin walitiliwa shaka kuwa  na ugonjwa huo, lakini baada  ya vipimo walibainika kuwa na magonjwa ya kawaida.

Hatimaye KenyaAirways yasitisha safari

Ebola:Hatimaye KenyaAirways yasitisha safari za ndege.
Hatimaye shirika la ndege la Kenya Airways limesalimu amri na kukubali shinikizo la kusitisha safari za ndege kuelekea mataifa matatu yaliyoathirika pakubwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Titus Naikuni alisema kuwa baada ya kupata ushauri wa shirikisho la Afya duniani WHO na wizara ya afya nchini Kenya shirikisho hilo limeamua kusimamisha safari zote za ndege kuenda Liberia na Sierra Leone.
Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia jumanne ijayo tarehe 19th Agosti 2014.
Hata hivyo shirika hilo lilisema kuwa litaendelea na safari zake kuelekea Nigeria.
Kama hatua za dharura abiria wote ambao walikuwa wamenunua tiketi za kuenda mataifa hayo watarejeshwa pesa zao .
Afisa Mkuu Mtendaji wa KQ anasema ni jambo la dharura kukomesha safari za ndege
Marufuku hiyo haitaathiri raiya wakenya ambao wanarejea nyumbani wala madaktari ama watu wanaoshiriki juhudi za kusimamisha mlipuko huo wa ugonjwa.
Shirika la ndege la KQ lilikuwa limepuza shinikizo la kusafiri kuenda Magharibi mwa Afrika hatua ambayo ilikuwa imevutia wadau nchini Kenya kutishia kuishtaki mahakamani ilikuishurutisha kukomesha safari hizo kwa hofu kuwa huenda ikasababisha kuenea kwa ugonjwa huo nchini Kenya.
Shirikisho la Afya duniani WHO lilizua hofu nchini Kenya lilipoitaja kama moja ya mataifa yenye athari kubwa ya kuenezwa kwa Ebola.
Ebola:Hatimaye KenyaAirways yasitisha safari za ndege.
Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ni kitovu muhimu cha usafiri wa ndege katika kanda ya Afrika Mashariki na kati .
Uwanja huo hupokea takriban ndege 76 kila wiki kwenda na kutoka Magharibi mwa Afrika.
Mapema juma hili athari ya ugonjwa huo wa Ebola ulipelekea shirika la ndege la Korea kusimamisha safari zake za ndege kuingia Kenya kwa hofu ya maambukizi ya Ebola.
Hadi kufikia sasa hakuna mkenya yeyote aliyepatikana na ugonjwa huo wa Ebola.
Watu zaidi ya 1000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo katika mataifa ya Sierra Leone Guinea Libera na Nigeria.

Thursday, 14 August 2014

Madaktari waunda masikio toka ubavuni

Madaktari waunda masikio toka ubavuni mwa kijana mwenye miaka 9
Madaktari nchini Uingereza wameumba masikio kutokana na ubavu wa kijana aliyezaliwa bila ya viungo hivyo muhimu.
Kijana huyo wa miaka tisa Kieran Sorkin alizaliwa bila masikio na madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya mbinu mpya ya matibabu katika hospitali ya Great Ormond Street iliyoko jijini London..
Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kuwa takriban watoto 100 huzaliwa bila kiungo hicho muhimu nchini Uingereza .
Madaktari wanaita ugonjwa huo microtia.
Kieran aliyezaliwa kama kiziwi hakuwa na masikio alipozaliwa badala yake alizaliwa na shimo mbili na ndewe tu badala ya masikio.
Tayari kieran anasikia baada ya upasuaji wa awli ambao ulimsaidia kupandikiza kifaa kinachomsaidia kupaza sauti ndani ya masikio yake.
"Ningependa watu wakome kuniuliza kwanini unakaa tofauti hivi ", alisema Kieran akiwa katika mtaa wa Hertfordshire.
"nimefurahishwa sana kufanana na marafiki wangu ''.
"Hata mimi ninafurahi kuwa sasa nitaweza kuvaa miwani na vifaa vya kusikizia muziki."
Madaktari waunda masikio toka ubavuni mwa kijana mwenye miaka 9
Mamake Kieran ,Louise Sorkin alisema kuwa kijana huyo ni mchangamfu sana na alikuwa anasubiri kwa hamu kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza masikio hayo.
"Sikuwa nafurahiwa watoto wenzake wakimkejeli kutokana na maumbile yake."
Asubuhi ya siku ya upasuaji huo Neil Bulstrode aliumba masikio hayo na akapandikiza akitumia teknolojia ya kisasa ya kushona masikio hayo chini ya ngozi ya kichwa chake .
Wanasayansi hao wanasema kuwa walitumia mbinu mpya ya kukuza viungo hivyo.
Kieran alifurahishwa sana alipooeshwa masikio yake mapya siku tatu baada ya operesheni hiyo.

Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.
Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.
Kuidhinisha utumizi wa dawa ilio katika majaribio ni swala gumu.
Dawa hiyo ambayo haijajaribiwa imetumiwa na raia wawili wa kutoa msaada kutoka marekani ambao afya yao imeimarika,lakini kasisi huyo wa Uhispania ambaye pia aliitumia dawa hiyo ameaga dunia.
Watu wasiopungua 1,013 wameaga dunia kutokana na kuambukizwa virusi hivyo katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Hatua hii ilichukuliwa huku Liberia ikitangaza kuwa ilihitaji kupata dawa la kufanyia majaribio liitwalo Zmapp baada ya kuiomba serikali ya Marekani.
Shirika la WHO lilisema kuwa lilikuwa limeombwa kupendekeza hatua hiyo kwa sababu ya kusambaa kwake na idadi kubwa ya vifo.
WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola
Shirika hilo lilisema kuwa mahali ambapo matibabu ya majaribio yanapofanyiwa panahitaji kuwa na ridhaa na matekeo ya jaribio hilo kukusanywa na kushiriki na wengine.
Katika ripoti iliyotolewa leo, shirika hilo linasema “Katika hali kama hizi za kuenea kwa ugonjwa huu, na iwapo masharti Fulani yataafikiwa, jopo hili limefikia makubaliano kuwa ni jambo la kimaadili kuingilia kati kwa mijarabu ambayo haijadhibitishwa huku ufanisi wake ukiwa haujulikani na adhari mbaya, kama matibabu au kinga.”
WHO ilitangaza kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kama janga la afya la dharura ulimwenguni.
Huku hayo yakijiri, serikari ya Liberia imesema kuwa madawa yatakayofanyiwa majaribio yatafikishwa nchini humo baadae juma hili – ingawa watengenezaji wa dawa madawa hayo Mapp Bio pharmaceutical walikuwa wameonya kuwa madawa hayo ni haba.
Zmapp imetumiwa kuwatibu wafanyikazi wawili wa US aid ambao walionyesha dalili ya kupata nafuu.
WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Padri mmoja wa kanisa la Roman Catholic, aliyeambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia, na ambaye aliaga dunia baada ya kurejea nyumbani kwao nchuni Uhispania pia amedhaniwa kuwa alikuwa amepewa dawa hizo.
Hata hivyo, dawa hizo zimejaribiwa kwa nyani tu na bado haijatathminiwa kuwa ni salama kwa binadamu.
Shirika la afya dunini WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Africa sasa imepita watu 1000.
Hii leo wataalam hao wa WHO wamekubaliana kwamba utumizi wa dawa hizo utakubalika iwapo kutakuwa na uwazi huku rukhsa ikitolewa na wote wanaoshiriki katika tiba hiyo mbali na kuficha siri ya mgonjwa aliyetibiwa.
Na huku hayo yakijiri Liberia ambalo ndio taifa lililoathiriwa sana na ugonjwa huo lilianza kutumia dawa hizo kutoka marekani kabla ya uamuzi wa utumizi wake kutolewa na WHO.

Kenya katika hatari ya kupata Ebola

Afisa wa shirika la afya duniani akieleza kuhusu janga la Ebola Duniani.
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na ndio hivi karibuni imeripoti kuwa na theluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katika hatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Serikali hata hivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi ya safari 70 za ndege kutoka Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.